Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa afuatilia taarifa za ajali ya helikopta ya Rais wa Iran
2024-05-20 14:50:20| cri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa taarifa kupitia msemaji wake akisema anafuatilia kwa karibu ripoti ya ajali ya helikopta iliyombeba rais wa Iran. Bw. Guterres anatumai kuwa Rais wa Iran na wasaidizi wake wako salama.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa kuhusu ajali hiyo iliyohusisha helikopta ya Rais Raisi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa helikopta iliyombeba Rais wa Iran, Waziri wa Mambo ya Nje na wafanyakazi wengine walioambatana nao ilipata ajali katika eneo la Varzhagan katika Mkoa wa Azerbaijan Mashariki. Licha ya hali mbaya ya hewa na mazingira magumu, vikosi vya uokoaji bado vinaendelea na kazi katika eneo la ajali hiyo.