Jeshi la Uganda limesema limemkamata kamanda wa kundi la waasi la ADF anayehusika na utengenezaji wa vifaa vya kulipika (IEDs) na kuwaokoa watu tisa waliotekwa nyara katika operesheni ya pamoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Msemaji wa jeshi la Uganda katika operesheni hiyo ya pamoja inayoitwa Operesheni Shujaa, Bilal Katamba, amesema wanajeshi wa Uganda, pamoja na wenzao wa DRC, wamemkamata Anywari Al Iraq katika eneo la Apumu, mkoa wa Ituri mashariki mwa DRC jumamosi iliyopita. Amesema katika opereheni hiyo, bunduki moja aina ya submachine, risasi 45, redio ya mkononi ya kupokea na kupeleka habari, na aina mbalimbali za malighafi za kutengenezea vifaa vya kulipuka pia vikilamatwa.