Rais wa China ampongeza Mahamat Idriss Deby Itno kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Chad
2024-05-21 19:46:30| CRI

Rais Xi Jinping wa China amemtumia salamu za pongezi Bw. Mahamat Idriss Deby Itno kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Chad.

Katika salamu hizo, rais Xi ameeleza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Chad umedumisha mwelekeo mzuri, uaminifu wa kisiasa kati ya pande hizo mbili umeongezeka, ushirikiano katika sekta mbalimbali umepata matokeo mazuri, na ushirikiano katika mambo ya kimataifa umeimarishwa.

Rais Xi amesisitiza kuwa, anaweka mkazo mkubwa katika kuendeleza uhusiano kati ya China na Chad, na kwamba angependa kushirikiana na rais mteule Mahamat kuimarisha kusaidiana na kuungana mkono, na kuhimiza ushirikiano wa kirafiki, ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.