Tanzania yang’ara ajenda ya maji kwa ustawi wa wote kwenye Kongamano la maji mjini Bali
2024-05-21 09:46:29| cri

Waziri wa Maji wa Tanzania Bw. Jumaa Aweso amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwenye Kongamano la 10 la Maji Duniani (10th World Water Forum) linalofanyika mjini Bali nchini Indonesia.

Kwenye mkutano wa Ngazi za Juu ulioongozwa na Rais wa Indonesia Joko Widodo, pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nchi mbalimbali Duniani, Tanzania imeithibitishia Dunia kuhusu utashi na uongozi wa kisiasa katika kutatua matatizo ya maji.

Baada ya Waziri wa Maji kuwasilisha kauli na tamko la Tanzania kwa niaba ya Rais Samia lililoelezea utekelezaji na mikakati inayoakisi kauli mbiu ya kongamano la Maji kwa ustawi wa pamoja, nchi mbalimbali zimeipongeza Tanzania kwa kazi kubwa inayoendelea kufanyika na mikakati iliyojiwekea hususani katika eneo la kufikisha huduma ya Maji vijijini.

 

.