Uchumi wa Kenya waongezeka kwa asilimia 5.6 katika mwaka 2023
2024-05-21 09:46:50| cri


Idara ya Takwimu ya Kenya (KNBS) jana imetangaza kuwa, uchumi wa nchi hiyo uliongezeka kwa asilimia 5.6 katika mwaka 2023.

KNBS imesema, kufufuka kwa sekta ya kilimo kulihimiza ongezeko hilo, kutokana na hali nzuri ya hewa iliyosaidia kuongeza mavuno ya mazao na mifugo.

Takwimu zimeonesha kuwa, katika mwaka 2023 sekta za kilimo, misitu na uvuvi nchini Kenya ziliongezeka kwa asilimia 6.5, ikilinganishwa na asilimia 1.5 ya mwaka 2022.