Mashirika kadhaa ya kimataifa mjini Geneva yasisitiza kuunga mkono kithabiti kanuni ya China moja
2024-05-21 20:57:06| cri

Ujumbe wa kudumu wa China kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva na mashirika mengine ya kimataifa nchini Uswisi umesema hivi karibuni mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa mjini Geneva yamesisitiza ahadi yao ya azimio nambari 2758 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuunga mkono kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja.

Kituo cha Kusini pia kimesisitiza kuwa kuna China moja tu duniani, Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya ardhi ya China, na serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ndiyo serikali pekee halali inayowakilisha China yote. Kituo hicho kinapinga aina yoyote ya "uhuru wa Taiwan" na inaunga mkono kikamilifu muungano wa amani wa China.