Viongozi wa Afrika walaani jaribio la mapinduzi lililoshindwa nchini DRC
2024-05-21 08:33:25| CRI

Viongozi wa nchi za Afrika na mashirika ya kikanda wamelaani vikali jaribio la mapinduzi lililotokea jumapili asubuhi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amelaani matumizi yoyote ya mabavu yanayolenga kubadili utaratibu wa kikatiba katika nchi yoyote ya Afrika, na kupongeza vikosi vya ulinzi na usalama vya DRC kwa kuzima jaribio hilo.

Nayo Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imeipongeza DRC kwa kudhibiti hali ambayo ilikuwa na uwezekano wa kuwa mbaya zaidi.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphoa amesema anafurahi kuona jaribio hilo la mapinduzi nchini DRC halikufanikiwa, kwani lingekuwa pigo kubwa sana kwa SADC.