Shirikisho la Kampuni za China nchini Tanzania (CEAT) limekabidhi vifaa vya muziki na michezo pamoja na majengo yaliyofanyiwa ukarabati ya Shule ya Msingi ya Urafiki kati ya China na Afrika iliyoko jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Kitila Mkumbo walihudhuria hafla hiyo.
Waziri Mkumbo amelishukuru Shirikisho hilo kwa msaada huo, na kusema elimu imeendelea kuwa kipaumbele katika mkakati wa Tanzania, na kuongeza kuwa msaada huo utawezeha shule hiyo kuongeza utendaji wake.
Naye Balozi Chen amelishukuru Shirikisho hilo kwa msaada huo, ambao utawawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri zaidi, na kuongeza kuwa serikali ya China daima imekuwa ikiunga mkono makuzi ya vipaji na maendeleo ya elimu nchini Tanzania.