Shirika la ndege la Ethiopia lazindua kituo kilichojengwa na China na kuongeza uwezo wake wa kuhudumia abiria
2024-05-21 22:41:02| cri

Shirika la ndege la Ethiopia limezindua kituo cha abiria cha ndani kilichojengwa na China mjini Addis Ababa. Kituo hicho kimejengwa kwa gharama ya dola milioni 50 na za Kimarekani kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, upanuzi wake umejumuisha kazi za ukarabati, utakaoongeza maradufu uwezo wa kubeba abiria wa kila mwaka wa kituo hicho.

Ofisa mkuu mtendaji wa Shirika la Ndege la Ethiopia Mesfin Tassew, amesema wakati wa hafla ya uzinduzi kwamba kituo hicho kitaunganisha mji wa Addis Ababa na vituo zaidi ya 20 vya ndani. Kituo hicho kitatumika kama kituo muhimu cha kuwezesha nchi hiyo kuhimiza mafungamano, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na kuhimiza sekta ya utalii.