Iran yaanza uchunguzi kuhusu kifo cha rais Raisi katika ajali ya ndege
2024-05-21 08:31:01| cri

Mnadhimu Mkuu wa jeshi la Iran Meja Jenerali Mohammad Bagheri ametuma ujumbe wa ngazi ya juu kuchunguza ajali ya helikopta iliyosababisha kifo cha rais wa nchi hiyo Ebrahim Raisi na ujumbe wake.

Taarifa zinasema, wajumbe hao wamefika katika eneo la ajali na kuanza uchunguzi, na matokeo yatatangazwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Serikali ya Iran jana ilithibitisha kuwa, Rais Raisi alifariki katika ajali ya helikopta iliyotokea jumapili.

Baraza la kulinda katiba la Iran lilitangaza siku hiyo hiyo kwamba, makamu wa kwanza wa rais wa Iran Bw. Mohammad Mokhber amechukua wadhifa wa rais hadi uchaguzi mpya wa rais utakapofanyika ndani ya siku 50 zijazo.