Uchaguzi wa rais mpya wa Iran kufanyika tarehe 28 Juni
2024-05-21 10:49:27| cri

Makamu wa kwanza wa rais wa Iran, mkuu wa bunge la Iran na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya sheria ya Iran tarehe 20 Mei waliunda kamati na kufanya mkutano wa kuweka mpango wa uchaguzi wa rais wa Iran.

Mkutano huo uliamua kuwa wagombea urais wataanza kujiandikisha Mei 30 hadi Juni 3, kampeni za urais zitafanyika kuanzia tarehe 12 hadi tarehe 27 Juni, na uchaguzi wa rais utafanyika tarehe 28 Juni.