Zaidi ya watu 40 wauawa katika shambulizi katikati mwa Nigeria
2024-05-22 08:31:18| cri

Zaidi ya watu 40 wameuawa na kundi la watu wenye silaha walioshambulia kijiji kimoja katika Jimbo la Plateau, nchini Nigeria Jumatatu.

Kamishna wa habari wa Jimbo la Plateau Bw. Musa Ibrahim Ashoms, amesema, kundi la watu wenye silaha waliokuwa wakiendesha pikipiki walivamia kijiji cha Zurak jumatatu usiku na kusababisha uharibifu mkubwa na kuua watu zaidi ya 40, na kuchoma moto nyumba kadhaa.