Biashara ya Tanzania yakua kwa asilimia 4.3, China ikiwa mshirika mkuu wa kibiashara
2024-05-22 22:40:12| cri

Sekta ya biashara nchini Tanzania ilikua kwa asilimia 4.3 mwaka 2023, huku nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Asia na Kusini mwa Afrika (SADC) zikiibuka kuwa washirika wakubwa wa biashara wa Tanzania.

Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Dk. Ashatu Kijaji amesema mwaka 2022 sekta hiyo ilikua kwa asilimia 3.9, na kuongeza kuwa mchango wa sekta ya biashara katika pato la Taifa ulikuwa asilimia 8.3 mwaka 2023, ikilinganishwa na asilimia 8.2 mwaka 2022.

Mauzo ya Tanzania katika nchi za Asia kwa mwaka 2023 zikiwemo China, India, Japan na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), yalifikia Sh7.48 trilioni.

Ingawa kiasi hicho ni pungufu kwa asilimia 31.6 kutoka mauzo ya nje ya thamani ya Sh10.9 trilioni mwaka 2022, nchi za Asia ziliendelea kuwa washirika wakuu wa biashara wa Tanzania.