Kampuni ya Startimes ya China yatajirisha wasanii wa filamu Tanzania
2024-05-22 09:41:44| cri

Zaidi ya filamu 120 za wasanii wa Tanzania zimenunuliwa na chaneli mpya ya St Swahili Plus iliyo chini ya Kampuni ya Startimes Media ya China kwa ajili ya kuoneshwa kwa watazamaji.

Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Kampuni ya Startimes, Bw. David Malisa amesema hatua hiyo hiyo yote ni kuunga mkono juhudi za wasanii, lakini pia ni kuhakikisha kuwa wanatoa burudani kwa Watanzania.

Amesema kampuni hiyo imeanzisha chaneli ambayo asilimia 60 ya maudhui yake yanatoka ndani ya nchi, ambayo ni fursa kwa wasanii kuuza kazi zao ili wao waweze kunufaika, na pia watazamaji waburudike.

Mwakilishi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Edward Nnko amewapongeza Startimes kwa kutoa fursa kwa Watanzania, akisema Kampuni hiyo imekuwa ikitoa nafasi kwa watu mbalimbali duniani kujifunza Kiswahili kupitia vipindi tofauti.