Sudan Kusini yajiunga na taasisi ya kikanda ya usimamizi wa uchumi mkuu
2024-05-22 08:35:20| cri


Sudan Kusini Jumanne ilisaini mkataba wa kujiunga rasmi na Taasisi ya Usimamizi wa Uchumi Mkuu na Fedha ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI). 

MEFMI ni shirika la kikanda la kiserikali linalosaidia kuandaa program maalum za kujenga uwezo kwa wateja wake katika maeneo ya kipaumbele ya madeni ya kigeni na usimamizi wa uchumi mkuu na usimamizi wa fedha ili kusaidia utulivu wa kiuchumi na kifedha katika nchi wanachama wake. 

Gavana wa Benki Kuu ya Sudan Kusini James Alic Garang, amesema uanachama katika MEFMI utaisaidia Wizara ya Fedha ya nchi hiyo katika suala la kujenga uwezo katika usimamizi wa madeni, uwazi wa madeni, kuripoti madeni, na kurekodi madeni. Pia utaisaidia Benki hiyo kaika makadirio ya uchumi na usimamizi wa hazina, ambayo ni muhimu kwa nchi hiyo.