Rais Kagame asema Umoja ni msingi wa maendeleo ya Rwanda
2024-05-22 09:40:59| cri

Rais Paul Kagame amesema umoja wa Wanyarwanda umekuwa msingi wa ujenzi mpya na maendeleo ya kiuchumi ya nchi baada ya mauaji ya kimbari ya 1994.

Rais alisema hayo Jumanne, Mei 21, kwenye Jukwaa la Usalama Duniani la 2024 linalofanyika Doha, Qatar. Rais Kagame alieleza juu ya safari ya upatanisho kutoka kwa Mauaji ya Kimbari ya 1994 na ukweli kwamba makaburi ya halaiki ya wahanga bado yanagunduliwa miongo mitatu baadaye.

Rais Kagame amesema jamii imekuwa ikipona, na ni jambo ambalo hawakutarajia kwamba lingeenda haraka namna hii.

Amesema serikali imekuwa ikifanya kazi pamoja kujaribu kuirejesha nchi pamoja - nchi ambayo iligawanyika sana, na watu wake kuchukiana, na hayo ndiyo maisha na siasa walizozoea. Lakini sasa ni kinyume chake, wanajenga umoja.