Reli iliyojengwa na China yaboresha biashara ya ndani na nje ya Ethiopia
2024-05-22 08:33:02| CRI

Reli inayounganisha nchi za Ethiopia na Djibouti iliyojengwa na China imepunguza kwa kiasi kikubwa muda na gharama za uchukuzi, hivyo kuimarisha biashara ya ndani na nje ya Ethiopia.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pamoja ya Reli ya SGR ya Ethiopia na Djibouti, Abdi Zenebe amesema, reli hiyo inazidi kupendelewa katika usafirishaji na uingizaji wa bidhaa, ambapo kwa sasa, zaidi ya asilimia 15 ua biashaa ya jumla ya ndani na nje ya Ethiopia inafanyika kupitia reli hiyo.

Amesema reli hiyo ni ya uhakika zaidi katika usafirishaji wa bidhaa muhimu zinazouzwa nje ya Ethiopia, ikiwemo kahawa, na kuongeza kuwa, asilimia 98 ya kahawa yote ya Ethiopia inayouzwa nje, inapita katika reli ya SGR inayounganisha nchi hiyo na Djibouti.