Somalia yazindua mashauriano kuhusu mpango mpya wa mabadiliko
2024-05-23 08:23:58| cri



 Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre jana amezindua mashauriano kuhusu Mpango mpya wa Mabadiliko ya Kitaifa (NTP), ambao ni mkakati mpya unaolenga kuboresha utawala nchini humo. 

Bw. Barre amesema mpango huo unalenga kuwekeza katika sekta za uzalishaji ili kutimiza ukuaji wa uchumi, kuongeza nafasi za ajira na fursa za maendeleo.

Bw. Barre amesisitiza kuwa mabadiliko ya maana yanaweza kupatikana tu wakati kila mtu anachukua hatua ya kutekeleza jukumu lake.