IGAD yatoa tahadhari ya mvua kubwa katika Pembe ya Afrika mpaka mwezi Septemba
2024-05-23 08:21:42| CRI

Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) imesema eneo kubwa la Pembe ya Afrika linatarajiwa kupata mvua kubwa kati ya mwezi Juni na Septemba mwaka huu.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya Mkutano wa 67 wa Mtazamo wa Hali ya Hewa katika Pembe ya Afrika ulioandaliwa na IGAD imesema, mvua zitakazonyesha kati ya mwezi Juni na Septemba zitakuwa kubwa zaidi ya kawaida katika za Djibouti, Eritrea, sehemu za katikati na kaskazini mwa Ethiopia, magharibi na katika pwani ya Kenya, na sehemu kubwa za nchi za Uganda, Sudan Kusini na Sudan.

Pia taarifa hiyo imesema, hali ya joto inaweza kuwa zaidi ya kawaida katika eneo hilo la Pembe ya Afrika, hususan kaskazini mwa Sudan, Kenya, Rwanda, Burundi na Tanzania.