Wanadiplomasua wapongeza FOCAC kwa kuimarisha uhusiano kati ya China na Afrika
2024-05-23 08:23:01| CRI

Wanadiplomasia wa Afrika wamesifiu Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwa kuimarisha uhusiano kati ya pande hizo mbili na kuboresha ushirikiano wa Kusini na Kusini.

Katika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu nafasi ya Ethiopia katika FOCAC uliofanyika mjini Addis Ababa nchini humo, wanadiplomasia hao wamesema majukwaa mengi ya uhusiano ambayo Afrika inayo hivi sasa, FOCAC inadumu kuwa jukwaa la maingiliano ya kimkakati zaidi na ya kina, upana na ngazi kubwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Balozi wa Ethiopia nchini China Tefera Derbew amesema, FOCAC ni matokeo ya juhudi za dhati za kuimarisha uhusiano wa China na Afrika, na linachukuliwa kama mfano wa ushirikiano wa Kusini na Kusini.

Amesema FOCAC inashikilia kanuni ya kutoingilia kati mambo ya nchi yoyote na kwa kiasi kikubwa inaendana na matarajio na vipaumbele vya Ajenda ya Mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika, huku lengo kuu likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kitamaduni.