Xi Jinping alituma barua ya pongezi kwa Kongamano la Kitaifa la Ushirikiano wa Viwanda na Uwekezaji kati ya China na GCC
2024-05-23 11:47:34| cri

Tarehe 23 Mei, Rais Xi Jinping alituma barua ya pongezi kwa Kongamano la Kitaifa la Ushirikiano wa Viwanda na Uwekezaji kati ya China na GCC.

Xi Jinping alisema kuwa mawasiliano ya kirafiki kati ya China na nchi za GCC yamedumu kwa maelfu ya miaka na yana historia ndefu. Mwaka 2022, mkutano wa kwanza wa wakuu wa China na GCC ulifanyika kwa mafanikio, na kuimarisha ushirikiano kati ya China na nchi za GCC. Kuzidisha ushirikiano wa viwanda na uwekezaji kati ya China na nchi za GCC kutasaidia kushirikisha pendekezo la "Ukanda na Barabara" na mikakati ya maendeleo ya nchi za GCC, kutoa mchango kwa pande zote, kuhimiza maendeleo mapya, na kukuza ustawi na maendeleo ya pande zote mbili. China inapenda kushirikiana na nchi za GCC ili kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya China na GCC.