Rais wa Zambia asisitiza ahadi ya kuimarisha ushirikiano na China
2024-05-23 08:21:00| CRI

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amethibitisha ahadi ya serikali yake ya kuimarisha ushirikiano na China.

Katika mazungumzo kati yake na Balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui, rais Hichilema ameipongeza China kwa msaada wake ikiwa ni pamoja na msaada wa kuunda mpya madeni, juhudi za kupambana na janga la COVID-19, na misaada iliyotoa wakati wa kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu hivi karibuni.

Kwa upande wake Balozi Du ameelezea matokeo mazuri ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, akitaja kukamilika kwa vifaa muhimu vilivyojengwa na China, na kiwango cha juu cha uwekezaji kati ya pande hizo mbili na biashara. Pia amesema anaamini kuwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili utaleta matokeo makubwa zaidi, na kuhimiza maendeleo yenye hali ya juu ya nchi hizo.