Mjumbe maalumu wa rais wa China ahudhuria hafla ya kumbukumbu ya marehemu rais wa Iran Ebrahim Raisi
2024-05-23 11:46:25| cri

Mjumbe maalumu wa Rais wa China Bw. Zhang Guoqing tarehe 22 Mei alihudhuria hafla ya kumbukumbu ya marehemu Rais wa Iran Ebrahim Raisi mjini Tehran, huku akikutana na kaimu rais wa Iran Mohammad Mokhber.

Bw. Zhang alisema rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha rais wa Iran Ebrahim Raisi, pia ametuma mjumbe maalumu kuhudhuria hafla ya maombolezo, kitendo ambacho kinaonyesha kuwa rais Xi na serikali ya China wanatilia maanani sana uhusiano kati ya China na Iran. China inaamini kuwa Iran itashinda changamoto ya muda, na kuendelea kuhimiza mambo mbalimbali ya kitaifa. Ameongeza kuwa marehemu Rais Ebrahim Raisi alitoa mchango mkubwa katika kulinda usalama na utulivu wa Iran na kuhimiza maendeleo na ustawi wa nchi, na kufanya juhudi kubwa katika kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Iran. China inapenda kushirikiana na Iran katika kuimarisha zaidi uhusiano huo.

Bw. Mokhber amemshukuru rais Xi kwa kutuma mjumbe maalumu kuhudhuria shughuli hiyo. Iran inapenda kushirikiana na China katika kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye sekta mbalimbali.