IMF yaidhinisha ufadhili wa dola za kimarekani 164m kwa Rwanda
2024-05-23 09:15:09| cri

Bodi ya Utendaji ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imeidhinisha jumla ya ufadhili wa dola za kimarekani milioni 164.6 kwa Rwanda. Taarifa iliyotolewa na IMF imesema, uamuzi huo umefikiwa baada mapitio ya utekelezaji wa Rwanda wa Chombo cha Uratibu wa Sera (PCI), ambacho ni mpango wa IMF kusaidia nchi kutekeleza sera za uchumi jumla zinazolenga kuzuia misukosuko na kujenga vizuizi dhidi ya majanga kutoka nje.

Uamuzi huo pia unafuatia mapitio ya utekelezaji wa nchi wa Mfumo wa Ustahimilivu na Endelevu (RSF) na Mfuko wa Kudumu wa Mikopo (SCF), ambayo yote ni vyombo vinavyotoa ufadhili kwa nchi ili kupambana na majanga ya tabianchi.