Rais wa Tanzania kuongoza mkutano Baraza la Amani na Usalama Afrika
2024-05-23 09:15:37| cri

Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika litakalofanyika Mei 25, 2024 jijini Dar es Salaam. Baraza hilo linafanyika wakati Tanzania inaendelea kutajwa kuwa kitovu cha harakati za ukombozi barani Afrika katika masuala ya amani, ulinzi na usalama.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. January Makamba amesema mkutano huo utakafanyika Mei, 24-25 kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Amesema kwa miaka mingi tangu Tanzania imepata uhuru, imekuwa ndio kitovu cha harakati za ukombozi barani Afrika, wapigania uhuru wa nchi nyingi za Afrika wakati wanatafuta uhuru na ukombozi wa nchi zao, waliitumia Tanzania kama sehemu ya kujipanga.