Rais Xi Jinping wa China afanya ziara ya ukaguzi mjini Rizhao, Shandong
2024-05-23 15:02:20| cri

Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara ya ukaguzi mjini Rizhao mkoani Shandong. Alitembelea bandari ya Rizhao na njia ya kijani ya pwani, ili kufahamu hali ya mji huo katika kuhimiza ujenzi wa bandari ya kisasa na kijani, kupanua ufunguaji mlango, kuimarisha urekebishaji na ulinzi wa ikolojia ya ufukweni, na kuinua kiwango cha maisha ya watu.