China yapenda kushirikiana na jamii ya kimataifa kuhimiza suluhisho la kina, haki na kudumu kwa suala la Palestina
2024-05-23 08:20:38| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema jana, China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa ili kuchukua jukumu la kiujenzi katika kumaliza mzozo wa Palestina na Israel mapema na kuhimiza suluhu la kina, haki na la kudumu kwa suala la Palestina.

Bw. Wang amesema, China imekuwa ikiunga mkono kithabiti haki za watu wa Palestina za kurejesha haki zao halali za kitaifa, kuunga mkono "suluhisho la nchi mbili", na ni moja ya nchi za kwanza kulitambua taifa la Palestina. Amesema China inaamini kuwa kipaumbele cha kwanza ni kutekeleza kwa ufanisi azimio namba 2728 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kusitisha mapigano mara moja na kumaliza vita, kumaliza mgogoro wa kibinadamu usio na kifani huko Gaza, na kurejea kwenye njia sahihi ya suluhisho la kisiasa la suala la Palestina.