Shindano la 23 la Daraja la Kichina kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Kigeni limefanyika jana jumatano jijini Dar es Salaam, Tanzania, na kushirikisha wanafunzi 11 kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini humo walioonyesha umahiri wao katika lugha ya Kichina.
Mshindi wa shindano hilo, Amani Njohole kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema, anatarajia kupanua zaidi uelewa wake wa lugha na utamaduni wa China, kwa kuwa matakwa yake ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kichina nchini Tanzania.
Njohole anatarajiwa kuja China baadaye mwaka huu kushiriki kwenye fainali za dunia za Shindano hilo.
Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema, shinano la Daraja la Kichina linalenga kuongeza ushawishi kwa vijana kutoka nchi zote kujifunza lugha ya Kichina, na kujenga jukwaa kwa mabadilishano ya lugha na utamaduni kati ya China na nchi nyingine.