FAO yakabidhi dozi milioni 2 za chanjo ya PPR kwa mbuzi, kondoo kwa Rwanda
2024-05-24 22:15:18| cri

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), limekabidhi dozi milioni mbili za chanjo kwa serikali ya Rwanda, kwa ajili ya kupambana na ugonjwa (PPR) unaowaathiri kondoo na mbuzi.

FAO imeisaidia Rwanda kuandaa na kupitisha Mkakati wa Kitaifa wa miaka sita wa Kudhibiti na Kutokomeza ugonjwa huo nchini Rwanda ifikapo 2030. Mkakati huo ambao pia uliowasilishwa kwa serikali ya Rwanda, pia unahimiza mbinu za kivumbuzi kutokomeza ugonjwa huo. Wakati ikikabidhi dozi milioni mbili za chanjo, FAO pia ilitoa msaada wa ziada wa kifedha na kiufundi kwa ajili ya utoaji wa chanjo ya PPR na kampeni za kuongeza ufahamu.