Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini aitaka serikali ya nchi hiyo kutekeleza mpango wa amani
2024-05-24 08:32:48| CRI

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Nicholas Haysom ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kutekeleza kikamilifu mpango mpya wa amani licha ya changamoto nyingi.

Memaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, Haysom amesema hayo alipohudhuria mkutano wa Tume Mpya ya Pamoja ya Usimamizi na Tathmini uliofanyika katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.

Amesema Haysom alitumia fursa hiyo kusisitiza haja ya dharura kwa serikali ya mpito kutekeleza kikamilifu makubaliano ya amani kutokana na hali mbaya ya kibinadamu na kiuchumi nchini Sudan Kusini.