Rais wa Guinea ya Ikweta kufanya ziara nchini China
2024-05-24 08:31:20| CRI

Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema Mbasogo atafanya ziara ya kitaifa nchini China kuanzia tarehe 26 hadi 31 mwezi huu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema anaamini kuwa ziara hiyo ya rais Obiang itaingiza msukumo mpya katika kusukuma mbele uhusiano wa kirafiki kati ya China na Guinea ya Ikweta kupata maendeleo kwa pande zote, na kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kupata matokeo mapya katika sekta mbalimbali.

Bw. Wang ameeleza kuwa, wakati wa ziara ya rais Obiang nchini China, atakutana na kufanya mazungumzo na rais wa China Xi Jinping na kushiriki kwa pamoja hafla ya kusaini nyaraka za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.