Rais mpya wa Chad aapishwa
2024-05-24 08:36:03| cri

Mohamed Deby ameapishwa jana kuwa rais wa Jamhuri ya Chad huko N'Djamena, mji mkuu wa nchi hiyo katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi na watu mashuhuri kutoka nchi mbalimbali.

Akihutubia mara baada ya kuapishwa, rais Deby amesema atajitolea kufanya mageuzi katika kipindi chake cha uongozi, kuendeleza uchumi imara, kuboresha mfumo wa afya, na kukuza maendeleo ya utamaduni na utalii wa nchi.

Habari zinasema, muda wa urais wa Mohamed Deby ni miaka 5 na anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano.