Msomi wa Afrika: Ziara ya Rais Xi Jinping yatia uhai mpya katika ushirikiano kati ya China na Ulaya
2024-05-24 16:05:46| CRI

Mwezi Mei mwaka huu, Ziara ya Rais Xi Jinping wa China barani Ulaya ilizua mjadala mkubwa duniani. Msomi wa Mali Profesa Yoro Diallo alipohojiwa hivi karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, amesema ziara hiyo imehimiza mshikamano na ushirikiano kati ya China na Ufaransa, Serbia na Hungary, imeelekeza mwelekeo sahihi wa uhusiano kati ya China na Ulaya, na kutia nguvu chanya kwa amani na maendeleo ya dunia.

 Prof. Diallo, ambaye ni mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa cha taasisi ya Utafiti wa Afrika Katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, amesema katika ziara hiyo ya Rais Xi Jinping, China na Ufaransa zimetoa taarifa nne za pamoja kuhusu Hali ya Mashariki ya Kati, Akili Bandia (AI) na Usimamizi wa Dunia, Anuwai ya Viumbe na Bahari, Mawasiliano na Ushirikiano wa Kilimo, na kusaini nyaraka zipatazo 20 za ushirikiano. China imekaribisha bidhaa nyingi zaidi za kilimo na vipodozi zenye ubora wa juu za Ufaransa kuingia kwenye soko la China, na juhudi za China kuelekea kuwa nchi ya kisasa zitatoa fursa nyingi zaidi mpya kwa makampuni ya nchi mbalimbali, ikiwemo Ufaransa. Matunda mengi yaliyopatikana katika ziara hiyo pia yamedhihirisha kuwa, Ufaransa inapenda kuimarisha mazungumzo na ushirikiano na China, na kuimarisha urafiki na kuaminiana kati ya China na Ufaransa na kati ya China na Ulaya kwa ujumla. Amesema, katika hali ya sasa ya kimataifa yenye utatanishi, maingiliano chanya kati ya China na Ufaransa yamethibitisha kuwa kuaminiana na kushirikiana kati ya pande hizo mbili kunaweza kutimizwa, hali inayoleta matumaini zaidi kwa jumuiya ya kimataifa.

 Prof. Diallo amesema, wakati alipotembelea Serbia, Rais Xi alitangaza hatua halisi za mwanzo za kuunga mkono ujenzi wa Jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Serbia. Hatua hiyo imeakisi dhamira ya China ya kuimarisha na kuinua Uhusiano wa Wenzi wa Kimkakati wa Pande Zote kati ya China na Serbia. Amesema, Hungary ni nchi ya kwanza ya Ulaya kusaini nyaraka za ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na China, na itakuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya kwa nusu ya pili ya mwaka huu. Prof. Diallo anaona, kuinuka zaidi kwa uhusiano kati ya China na Hungary, kutasaidia kutuliza uhusiano kati ya China na Ulaya, na kutia uhai mpya kwenye ushirikiano kati ya pande hizo mbili.