Raia kutoka Kenya, India ni kati ya 11 waliokufa kwenye ajali ya kiwanda cha sukari Tanzania
2024-05-24 10:16:25| cri

Raia kutoka Kenya na India ni miongoni mwa watu waliofariki katika ajali ya kiwanda cha sukari cha Mtibwa mkoani Morogoro. Maofisa wa zimamoto wa mkoa wa Morogoro wamesema ajali hiyo ilitokea kufuatia hitilafu ya umeme kwenye mfumo wa kupasha joto, na wamethibitisha kuwa Mkenya mmoja, Raia wa India na Mbrazil mmoja wamefariki dunia katika tukio lililotokea alfajiri ya Mei 23.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema waliopoteza maisha wote ni mafundi wa umeme na mashine waliokuwa kwenye chumba cha udhibiti wakiendelea na shughuli zao za mwisho kabla ya kuanza kwa zamu ya uzalishaji siku hiyo.