Uzalishaji wa umeme kwa nishati ya maji nchini Kenya waongezeka
2024-05-24 09:03:48| cri



Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Uchumi na Mkakati kwenye Nishati na Petroli nchini Kenya Bw. John Mutua jana amesema, kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha maji katika mabwawa, uzalishaji wa umeme kwa nishati ya maji nchini Kenya umeongezeka hadi MW 698 kutoka MW 536.

Bw. Mutua amewaambia waandishi wa habari huko Nairobi kuwa mvua kubwa iliyonyesha nchini humo katika miezi michache iliyopita imeongeza uzalishaji wa umeme kwa nishati ya maji kutoka kwa mabwawa ya Seven Forks yaliyoko mashariki mwa nchi hiyo.

Bw. Mutua amesema, kutokana na mvua nyingi, uzalishaji wa umeme kwa nishati ya upepo umepungua, na nafasi yake imechukuliwa na uzalishaji wa umeme kwa nishati ya maji.