Duru hii ya mgogoro kati ya Palestina na Israel yasababisha vifo vya watu 35,800 katika Ukanda wa Gaza
2024-05-25 21:55:24| cri

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na idara ya afya katika Ukanda wa Gaza, operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza katika siku iliyopita zimesababisha vifo vya watu 91 na wengine 210 kujeruhiwa. Tangu mgogoro wa Wapalestina na Israel uanze tarehe 7 Oktoba mwaka jana, idadi ya vifo vya watu katika Ukanda wa Gaza imefikia elfu 35 na mia 8, na idadi ya waliojeruhiwa imefikia elfu 80 na mia 2.

Idara ya afya ya Ukanda wa Gaza imetoa taarifa ikisema kutokana na kukaribia kuishiwa na mafuta ya jenereta, Hospitali ya Al-Aqsa huko Deir al-Bayrah, katikati mwa Ukanda wa Gaza italazimika kusitisha huduma baada ya saa chache, na wagonjwa mahututi na watu waliojeruhiwa maisha yao yatakuwa hatarini. Hospitali ya Al-Aqsa kwa sasa ndiyo hospitali pekee inayofanya kazi katika Ukanda wa Gaza.