Wanawake wajasiriamali na changamoto wanazokumbana nazo
2024-05-25 09:00:57| CRI

Mwishoni mwa miaka ya 1970, China ilianza kutekeleza sera ya mageusi na kufungua mlango. Sera hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwa jamii ya Wachina, hususan wanawake. Katika miaka kadha iliyopita, ilizoeleka kuwa wanawake jukumu lao ni kutunza familia, na hawakuwa na wajibu wa kutafuta pesa kwa ajili ya matumizi ya familia. Lakini katika zama hizi, kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, wanawake katika nchi mbalimbali hawajabaki nyuma na wanashiriki vyema katika shughuli mbalimbali za uchumi na maendeleo. Ujasiliamali ni jambo ambalo wengi wanapenda kufanya, na baadhi wanafanikiwa na kujikwamua kutoka umasikini. Miongoni mwao ni wanawake ambao zamani hawakupewa fursa za kushughulika na mambo ya ujasiliamali. Wanawake wengi wanakumbana na changamoto nyingi pale wanapoamua kujiajiri.

Hiyo ni kweli, lakini pia kuna ambao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika biashara zao, kwani wameweza kukabiliana na changamoto na kupata ufumbuzi, na hivyo kubadili maisha yao. Katika kipindi hiki cha Ukumbi wa Wanawake leo hii tutazungumzia wajasiriamali wanawake na changamoto wanazokumbana nazo, na pia tutakuwa na Simulizi inayomhusu mwanamke kutoka mkoa wa Xinjian anayeitwa Samira Arkin, mfanyabiashara wa nguo za harusi.