Mjumbe maalumu wa rais wa China ahudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais wa Comoro
2024-05-27 09:05:37| CRI

Kutokana na mwaliko wa rais wa Comoro Azali Assoumani, mjumbe maalumu wa rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa Bw. He Baoxiang amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais Assoumani tarehe 26 mwezi huu. Siku moja kabla ya hafla hiyo, alikutana na rais Assoumani katika mji wa Moroni, nchini Comoro.

Bw. He amefikisha pongezi na matumaini mema ya rais Xi Jinping kwa rais Assoumani akieleza kwamba China inatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya China na Comoro na inapenda kufanya juhudi pamoja na Comoro katika kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kati ya marais wa nchi hizo mbili, kuunga mkono kithabiti kila upande kulinda maslahi yake makuu, kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na kuimarisha ushirikiano halisi katika sekta mbalimbali.

Naye Rais Assoumani amemshukuru rais Xi kwa kutuma mjumbe maalumu kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwake, na kusema kuwa Comoro inashukuru uungaji mkono wa China katika juhudi yake ya ujenzi wa taifa na itaendelea kushikilia kithabiti kanuni ya“China Moja”, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na kuhimiza uhusiano huo ufikie ngazi ya juu zaidi.