Waziri mkuu wa China ahudhuria mkutano wa 9 wa Viongozi wa China, Japan na Korea Kusini
2024-05-27 22:12:34| cri

Tarehe 27 Mei asubuhi, waziri mkuu wa China Bw. Li Qiang, rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini na waziri mkuu wa Japan Bw. Fumio Kishida wamehudhuria mkutano wa 9 wa Viongozi wa China, Japan na Korea Kusini mjini Seoul, Korea ya Kusini. Taarifa ya pamoja imetolewa kwenye mkutano huo, ikisisitiza kuhimiza ujenzi wa utaratibu wa ushirikiano, na kulinda amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa dunia kwa pamoja.