Wakuu wa Bahrain, Misri, Tunisia na Umoja wa Falme za Kiarabu kuzuru China
2024-05-27 14:10:35| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, Mfalme Hamad bin Isa Al Khalifa wa Bahrain, rais Abdel Fattah El Sisi wa Misri, rais Kais Saied wa Tunisia na rais Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) watafanya ziara nchini China kuanzia tarehe 28 mwezi huu hadi Juni Mosi.

Amesema marais hao pamoja na mwenyeji wao rais wa China Xi Jinping, watahudhuria Sherehe ya Ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu.