Rais Xi Jinping ajibu barua alizoandikiwa na wawakilishi wa wanafunzi wa lugha ya Kichina nchini UAE
2024-05-27 08:57:51| CRI

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni amejibu barua alizoandikiwa na wawakilishi wa wanafunzi wa mradi wa elimu ya lugha ya Kichina wa “Shule Mia Moja” nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), akiwahamasisha kujifunza vizuri lugha hiyo na kuifahamu China, na kutoa mchango katika kuhimiza urafiki kati ya nchi hizo mbili.

Rais Xi amesema anafurahia kuona mkondo mpya wa kujifunza lugha ya Kichina nchini UAE, huku wanafunzi hao wakiwa mabalozi wadogo wa kuhimiza mawasiliano kati ya China na UAE.

Rais Xi amewakaribisha wanafunzi hao kuja China kuangalia Panda na kupanda Ukuta Mkuu, pamoja na kusoma katika vyuo vikuu vya China.

Pia amewakaribisha wanafunzi wengi zaidi wa UAE kujifunza Kichina na kuifahamu China, akitumai kuwa wao na wenzao wa China watawasiliana na kufunzana, na kupanda mbegu za urafiki mioyoni mwao na kutoa mchango katika kujenga siku zijazo za uhusiano kati ya China na UAE.