Hafla ya Siku ya Afrika iliyoandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje ya China na Ujumbe wa Ubalozi wa nchi za Afrika nchini China imefanyika Jumamosi iliyopita mjini Beijing.
Katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Chen Xiaodong amesema, mkutano ujao wa Baraza la Ushirikiano Kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika mwaka huu ambao muhimu kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili. Amesema China ingependa kushirikiana na Afrika kuchukua fursa hiyo kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo chini ya mfumo wa kujenga kwa pamoja Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na mapendekezo makuu matatu ya kimataifa, na kujenga Jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja kwenye kiwango cha juu zaidi.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa Mabalozi wa nchi za Afrika nchini China ambaye pia ni Balozi wa Cameroon nchini China Bw. Martin Mpana amesema, Afrika inapenda kudumisha ushirikiano wa karibu na China, na kuandaa kwa pamoja mkutano ujao wa FOCACna kusisitiza kwamba mabalozi hao wanashikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja.