Mjumbe wa China asifu uhusiano usiovunjika na Zambia
2024-05-28 09:13:56| CRI

Mshauri wa uchumi na biashara katika Ubalozi wa China nchini Zambia Bw. Liu Guoyu amesifu ushirikiano usiovunjika kati ya China na Zambia katika miaka iliyopita na kueleza imani yake kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaendelea kukua katika siku zijazo.

Akiongea kwenye hafla ya kuzindua mradi wa maboresho ya barabara inayoelekea Hospitali ya Mafunzo ya Chuo Kikuu cha Levy Mwanawasa iliyojengwa kwa ufadhili wa China mjini Lusaka, Bw. Liu Guoyu amesema, China itaendelea kuiunga mkono Zambia kwa kukuza mambo ya kisasa, kuboresha maisha ya Wazambia na kutimiza maendeleo na ustawi kwa pamoja.

Mradi huo wa barabara iliyopewa jina jipya la Barabara ya Urafiki kati ya Zambia na China, umefadhiliwa na Shirikisho la Wachina nchini Zambia.