Mkoa wa Gaza wa Msumbiji warejesha uzalishaji wa ngano kupitia uungaji mkono wa kiteknolojia wa China
2024-05-28 09:05:24| CRI

Mkoa wa Gaza, kusini mwa Msumbiji unatarajiwa kurejesha uzalishaji wa ngano katika robo hii ya mwaka, ukisaidiwa na teknolojia ya China kupitia kampuni inayowekezwa na China.

Kikimnukuu gavana wa mkoa huo Margarida Chongo, kituo cha Redio Msumbiji kimesema, upandaji wa kwanza unapangwa kuanza ndani ya siku kadhaa katika Eneo la Umwagiliaji maji la Lower Limpopo huko Xai-Xai, mji mkuu wa mkoa wa Gaza.

Gavana huyo amesema, katika kipindi cha kwanza, hekta zaidi ya 150 za shamba zitalimwa ngano. Urejeshaji wa uzalishaji wa ngano katika mfumo wa umwagiliaji wa maji wa Lower Limpopo umetimizwa baada ya karibu miaka 50 kupitia ushirikiano wa teknolojia ya China iliyotolewa na kampuni ya Wanbao.