Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC yajadili masuala ya maendeleo na fedha
2024-05-28 08:41:19| CRI

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imejadili kuhusu sera na hatua za kuharakisha maendeleo ya eneo la kati la China katika zama mpya, na vifungu vya sheria vya majaribio vya uwajibikaji wa kushindwa kuzuia au kuondoa hatari za kifedha.

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping, ameongoza mkutano ambao umetaka juhudi za kuharakisha maendeleo ya eneo la kati ikiwemo mikoa ya Shanxi, Anhui, Jiangxi, Henan, Hubei na Hunan zipigie hatua muhimu zaidi.