Korea Kaskazini yashindwa kurusha satelaiti ya upelelezi ya kijeshi
2024-05-28 14:38:11| cri

Shirika la Habari la Korea Kaskazini limesema, jaribio la kurusha satelaiti ya upelelezi lililofanywa na nchi hiyo jana jumatatu limeshindwa.

Ripoti iliyotolewa na Shirika hilo imesema, Idara ya Kitaifa ya Teknolojia ya Anga ya Juu ya Korea Kaskazini ilijaribu kurusha satelaiti ya upelelezi Malligyong-1-1 kwa kutumia roketi mpya ya kurushia satelaiti katika Kituo cha Kurushia Satelaiti cha Sohae kilichoko Kaunti ya Cholsan, mkoa wa Phyongan.

Shirika hilo limemnukuu ofisa mmoja wa Idara husika akisema kuwa, satelaiti hiyo ilishindwa kuruka kutokana na mlipuko wa hewa katika roketi hiyo wakati wa ngazi ya kwanza ya utaratibu wa kurusha satelaiti.