Madaktari wa China watoa huduma za matibabu bila malipo kwa wagonjwa wa Zanzibar nchini Tanzania
2024-05-28 10:12:34| CRI

Kundi la 33 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar lilitoa huduma za matibabu bila malipo kwa wagonjwa zaidi ya 100 katika maeneo ya vijijini wiki iliyopita.

Naibu mkuu wa timu hiyo Bw. Li Guang, alisema Jumatatu kwamba huduma za matibabu bure zilitolewa Alhamisi kwa watu wa vijiji vya Chambani kisiwani Pemba. Madaktari hao walitoa ushauri kwa wagonjwa hao kuhusu tathmini ya afya, matibabu ya ndani, upasuaji, magonjwa ya wanawake, watoto, magonjwa ya masikio na koo na mifupa, na kuongeza kuwa pia wamepima shinikizo la damu, sukari ya damu, ushauri wa kiafya, matibabu ya dharura na huduma nyinginezo, na kusambaza dawa bila malipo.

Bw. Li alisema madaktari hao pia waliwaelimisha wanawake wa eneo hilo kuhusu upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi na kuwahimiza kwenda hospitalini hapo kwa uchunguzi wa kimatibabu bila malipo.