Mkutano wa 9 wa Viongozi wa China, Japan na Korea Kusini umefanyika jana huko Seoul, mji mkuu wa Korea ya Kusini, na kutoa taarifa ya pamoja, ikisisitiza kuhimiza ujenzi wa utaratibu wa ushirikiano, na kulinda amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa dunia kwa pamoja.
Wachambuzi wanaona kuwa, wakati dunia inapokabiliwa na misukosuko na kudidimia kwa uchumi, mkutano huo unaonesha kuwa nchi hizo tatu zinatilia maanani na kuthamini ushirikiano. Katika siku zijazo, nchi hizo zinapaswa kuepuka usumbufu wa nje, na kuheshimu maslahi ya kila upande na ufuatiliaji mkuu, ili kuanzisha upya ushirikiano kati yao, hatua ambayo si kama tu itawanufaisha wananchi wao, bali pia itakaribishwa na nchi za kikanda na dunia nzima.