Baraza la Afya Duniani lakataa kwa mara nyingine tena pendekezo linalohusiana na Taiwan
2024-05-28 08:40:34| CRI

Baraza la Afya Duniani (WHA), chombo cha juu zaidi cha maamuzi cha Shirika la Afya Duniani (WHO), Jumatatu liliamua kutojumuisha katika ajenda yake pendekezo la ushiriki wa Taiwan katika mkutano wa kila mwaka kama mwangalizi.

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva na mashirika mengine ya kimataifa nchini Uswisi, Chen Xu, alisema katika taarifa yake kwamba msimamo wa China kuhusu ushiriki wa Taiwan katika WHA ni thabiti na wazi. Suala hilo lazima lishughulikiwe chini ya kanuni ya China moja, ambayo pia ni kanuni ya msingi iliyoidhinishwa katika Azimio namba 2758 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) na Azimio la 25.1 la WHA.

Ameongeza kuwa mamlaka ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo inashikilia msimamo wa ufarakanishaji wa "Taiwan kujitenga na China," ili msingi wa kisiasa wa ushiriki wa eneo la Taiwan katika baraza hilo usiwepo tena.

Chen alibainisha kuwa serikali kuu ya China imefanya mipango ifaayo kwa ajili ya ushiriki wa eneo la Taiwan katika masuala ya afya duniani chini ya kanuni ya China moja.