Watu wenye silaha wawaua watu saba na kuwateka nyara zaidi ya 150 katikati mwa Nigeria
2024-05-28 09:02:02| CRI

Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti kuwa watu wasiopungua saba wakiwemo walinzi wanne wameuawa huku wengine zaidi ya 150 wakitekwa nyara wakati watu wengi wenye silaha walipofanya mashambulizi huko Kuchi, eneo la Munya katika jimbo la Niger nchini humo.

Mkuu wa serikali ya mitaa ya Munya, Aminu Najume amesema kuwa washambuliaji hao wanaoshukiwa kuwa majambazi walikwenda nyumba kwa nyumba kuchagua mateka wao. Ameelezea masikitiko yake juu ya mashambulizi ya mara kwa mara yanayotokea huko Munya na kutaka serikali iimarishe hatua za usalama dhidi ya majambazi wanaotishia maisha ya wakazi wa eneo hilo.